Simba kamili gado Afrika Kusini, Niyonzima, Okwi wakujiunga na timu
Nyota wawili wa kutumainiwa katika kikosi cha Simba ambao
usajili wao klabuni hapo hivi karibuni ulikuwa gumzo, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima pamoja na Mganda,
Emmanuel Okwi wanatarajia kujiunga na timu hiyo kesho Jumamosi huko Afrika
Kusini.
Kikosi cha Simba kipo nchini humo kikijifua kwa ajili ya
msimu ujoa wa Ligi Kuu Bara unaotarajia kuanza kutimua vumbi Agosti 26, mwaka
huu lakini pia michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba, zimedai kuwa
wachezaji hao watajiunga na timu hiyo baada ya kumalizika kwa masuala yao
mbalimbali yalioyokuwa yakiwakabili.
“Niyonzima alikuwa akikabiliwa na suala la kimkataba
kwani mkataba wake na Yanga ulikuwa uhajamalizika lakini leo Julai 28 ndiyo
unafikia tamati hivyo kesho, Jumamosi atajiunga na timu huko Afirika Kusini baada
ya kuwa huru.
“Tiketi yake ya safari tumemtumia tangu siku ya Jumanne,
lakini pia Okwi naye atajiunga na timu hiyo kesho kutokana na kumalizika kwa
zoezi la utoaji wa tuzo kwa wachezaji wa Uganda waliofanya vizuri katika ligi
kuu ya nchi hiyo.
“Zoezi hilo ndilo lililomchelewesha kujiunga na timu kwa
sababu alikuwa akiwania tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya nchini hiyo, hata
hivyo leo hii ameondoka na tayari ameshafika Afrika Kusini,” kilisema Chanzo
hicho cha habari.
No comments: