CONTE KUJA NA ‘SURPRISE’ LIGI YA MABINGWA ULAYA
KOCHA
Mkuu wa Chelsea, Antonio Conte, amesema kesho Jumanne atafanya ‘surprise’ pale
kikosi chake kitakapokuwa mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi
ya Qarabag FK ya Azerbaijan.
CONTE |
Conte
amepanga kufanya surprise hiyo kwa kuwachezesha wachezaji tofauti na
waliozoeleka ili kupata muda wa kuyapumzisha majembe yake kwa ajili ya
kuyatumia wikiendi ijayo pale watakapokuwa na kibarua cha kupambana na Arsenal.
WACHEZAJI WA CHELSEA |
“Itanilazimu
kubadili kikosi, kucheza mechi saba ndani ya siku 21 si kitu rahisi,” alisema
Conte na kuongeza.
“Kipindi
cha nyuma kabla ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, nilikuwa nawapumzisha wachezaji
wangu, lakini kwa England ni ngumu kuwapumzisha wachezaji muhimu. Unaweza
kuchezesha timu ya kawaida na ukapoteza.
“Tumecheza
mechi mbili tayari, kisha inafuata mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kisha dhidi
ya Arsenal Jumapili, halafu tunacheza Kombe la Carabou, halafu mechi zingine
mbili za ligi kuu kabla ya kukutana na Atletico Madrid.”
No comments: