Tambwe arejea uwanjani kuiokoa Yanga
Straika wa kimataifa wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe tayari ameanza mazoezi
mepesimepesi baada ya kupata nafuu ya tatizo la goti lililokuwa likimsumbua kwa
muda.
Tambwe
alipata tatizo hio hivi karibuni wakati alipokuwa na timu hiyo Kisiwani Pemba akijiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii
dhidi ya Simba ambayo iliyofanyika siku chache zilizopita.
Tambwe amesema hivi sasa anaendelea vizuri baada ya
kupata matibabu na tayari ameshaanza kufanya mazoezi mepesimepesi ya gym chini
ya jopo la madakitari wa Yanga.
Amesema
anajitahidi kuzingatia maelekezo yote anayopewa na madaktari hao ili aweze
kurejea uwanjani mapema kwa ajili ya kuiongoza timu hiyo kuibuka na ushindi
katika mechi zake zote za ligi kuu lakini pia kuishusha Simba kutoka katika
nafasi ya kwanza ambayo inaishilia hivi sasa.
No comments: