REKODI ZA MESSI ZILIZOJIFICHA HIZI HAPA
STAA wa Barcelona, Lionel Messi, anajulikana ni bingwa wa kuweka rekodi. Katika rekodi hizo zipo ambazo wengi wanazifahamu na zingine hazifahamiki na wengi. Zile ambazo hazifahamiki na wengi ni hizi hapa:
Msimu wa 2011/12 alifunga mabao 50 katika La Liga ikiwa ni
idadi kubwa ya mabao kuyafunga ndani ya msimu mmoja.
Katika La Liga amefunga mabao 359 ambayo ni idadi ya juu
zaidi kuliko mchezaji yeyote.
Kwenye ngazi ya klabu, Messi ni mchezaji aliyeshinda makombe
mengi zaidi yanayotambulika ambayo ni 29.
Mabao mengi zaidi kwa msimu mmoja kwa michuano yote
anaishikilia yeye akiwa na mabao 91.
Pamoja na kuwa hajawahi kubeba Kombe la Dunia, Messi ndiye
mchezaji mwenye mabao mengi zaidi timu ya taifa ya Argentina baada ya kupachika
61.
No comments: