UTAMU WA FDL WIKIENDI HII HUU HAPA
RAUNDI ya Sita ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL), itaendelea wikiendi hii kwa kupigwa mechi kadhaa kwenye viwanja tofauti.
Katika Kundi A, Mvuvumwa FC ya Kigoma, watacheza na Mgambo
JKT katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mechi nyingine kwenye kundi hilo itafanyika kesho Jumapili
Oktoba 22, mwaka huu kwa michezo mitatu.
Mechi hizo ni kati ya Kiluvya United na Mshikamano kwenye Uwanja wa Filbert Bayi, Pwani. African
Lyon itacheza na Ashanti United kwenye Uwanja wa Uhuru, wakati Friends
Rangers itapambana na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Azam, Dar es Salaam.
Katika Kundi B, leo Jumamosi, Mbeya Kwanza itacheza na JKT
Mlale katika Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi, Pwani na Jumapili Polisi Tanzania
watawakaribisha KMC kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi, huku Mawenzi Market wakiwaalika
Mufindi United kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Katika Kundi C, michezo ya leo Jumamosi itazikutanisha Biashara Mara dhidi ya JKT
Oljoro kwenye Uwanja wa Karume, Mara, Transit Camp itakuwa mwenyeji wa Dodoma
FC kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, huku Toto Africans ya Mwanza
itacheza na Rhino Rangers ya Tabora
katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
No comments: