SIMBA YAIPIGA NJOMBE 4G, OKWI HAKAMATIKI
LIGI Kuu Tanzania Bara raundi ya saba, imeendelea leo Jumamosi baada ya jana Ijumaa Mwadui FC kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera Sugar katika Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
Katika michezo ya leo Jumamosi ambayo ilikuwa sita, Simba
ikiwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar, imeibuka na ushindi wa mabao 4-0. Mabao
ya Simba yamefungwa na Emmanuel Okwi, Laudit Mavugo na Mzamiru Yasin aliyefunga
mawili. OKwi amefikisha mabao nane na kuendelea kukaa kileleni kwa ufungaji.
Mbao FC ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa CCM Kirumba,
ilishindwa kufungana na Azam FC, huku Lipuli ikiichapa Majimaji bao 1-0 katika
Uwanja wa Samora mjini Iringa.
OKWI |
Mbeya City wameutumia vema uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine
baada ya kuinyuka Ruvu Shooting mabao 2-0, Ndanda na Singida United zilishindwa
kufungana kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, huku Mtibwa Sugar ikiichapa
Prisons bao 1-0 kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
KIKOSI CHA MTIBWA |
Ligi hiyo itaendelea tena kesho Jumapili kwa kupigwa mchezo
mmoja kati ya Stand United na mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Yanga. Mchezo huo
utapigwa katika Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
No comments: