Begi lamzuia Mghana wa Simba kufanya mazoezi
WAKATI
Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog akijipanga kumtumia mshambuliaji
wake mpya raia wa Ghana, Nicholaus Gyan dhidi ya Azam FC, mchezaji huyo juzi
Jumamosi alishindwa kufanya mazoezi na timu hiyo kwa sababu ya begi.
Gyan
ambaye amesajiliwa na Simba hivi karibuni akitokea Ghana hakuweza kufanya
mazoezi na timu hiyo baada ya kukosa vifaa vya mazoezi kutokana na kupotelewa
na begi lake liliokuwa na vifaa hivyo pamoja na nguo zake za nyumbani wakati alipokuwa
safarini akitokea kwao nchini Ghana.
Kutokana
na hali hiyo alijuka akiwa mtazamaji wakati wachezaji wenza wa Simba walipokuwa
wakijifua kwa ajili kujiandaa na mechi
yao ya ligi kuu dhidi ya Azam ambayo awali ilikuwa imepangwa kufanyika Jumatano
hii lakini sasa imesogezwa mbele mpaka Jumamosi, Septemba 9, mwaka huu.
Gyan
amekumbana na balaa hilo Jumamosi alfajiri baada ya kutua katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA) akitokea Ghana
ambapo hakuweza kuliona begi lake hilo.
Kitendo
hicho kinadaiwa kumvuruga vilivyo jambo ambalo pia lilimsikitisha Omog ambaye
alikuwa akimusubilia kwa hamu kubwa mchezaji huyo katika mazoezi hayo.
Omog
alisema kuwa uongozi wa timu hiyo unalishugurikia suala hilo ili Gyan aweze
kupata begi lake hilo lakini pia kwa upande wake yeye anajipanga kuhakikisha ana
mweka sawa kiakili ili aweze kumtumia
kwenye mechi hiyo dhidi ya Azam.
“Taarifa
za kupotelewa begi lake nimezisikia lakini najua uongozi utakuwa
unalishugurikia ila binafsi nimefurahia ujio wake na sasa najipanga kuhakikisha
anakuwa sawa kwa ajili ya mechi yetu dhidi ya Azam.
“Niniajitahidi
kumweka sawa kiakili ili aweze kusau suala hilo lilomtokea kabla ya kukabiliana
na Azam, kwani tunakata kupata ushindi dhidi yao ili tuendelea kuwa juu katika
msimamo wa ligi,” alisema Omog
Chanzo:
Championi
No comments: