Tambwe, Chirwa wawatuliza Yanga
WASHAMBULIJI wa kutumainiwa wa Yanga, Obery Chirwa pamoja na
Amissi Tambwe leo hii wataungana na kikosi hicho mazoezi ya kujiandaa na mechi
yao Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Yanga na Njombe Mji zitapambana Jumamosi ijayo katika Uwanja
wa Sabasaba mijini Njombe baada ya Shirikisho la Soka Tanzania kuifanyia
mabadiliko ratiba ya ligi kuu ambapo awali ilikuwa zipambane Jumatano hii.
Kitendo hicho cha nyota hao kujiunga na kikosi hicho
kimepokelewa kwa mikono miwili na viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo
baada ya kuwakosa kwa kipindi kirefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya
goto.
Majeraha hayo yaliwafanya wawe nje ya uwanja kwa kipindi
kirefu huku wakishindwa kuitumikia timu yao hiyo katika mchezo wa Ngao ya Jamii
dhidi ya Simba lakini pia ule wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli FC.
Daktari wa Yanga, Edward Bavu alisema kuwa wachezaji hao kwa
pamoja leo hii waanza mazoezi baada ya kupona majeraha yao.
“Hakika tunamshukuru Mungu kwa hilo kwani, kwani wamerejea
katika kipindi muafaka baada ya kupona majeraha yao gati.
“Kwa hiyo, mpaka kufikia hapa kazi iliyobakia ni kwa makocha
kuhakikisha wanawapatia mazoezi ya ufiti kabla ya kuanza kuwatumia katika mechi
zijazo,” alisema Bavu na kuongeza kuwa.
“Wachezaji ambao tutaendelea kuwakosa ni kikosini kwetu ni
kipa Beno Kakolanya na Geofrey Mwashiuya ambao wote bado ni majeruhi na
wanaendelea na matibabu,” alisema Bavu.
Chanzo:
Championi
No comments: