Ubelgiji yatisha amani Ulaya
Timu ya soka taifa ya Ubelgiji imekuwa ya kwanza kutoka Ulaya kujiunga na
wenyeji Urusi katika kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia baada ya kupata
ushindi dhidi ya Ugiriki wa 2-1 kupitia mabao kutoka kwa Jan Vertonghen na
Romelu Lukaku.
Mabao yote matatu yalifungwa katika dakika tano kipindi cha pili,
Vertonghen akitangulia kwa kuiweka Ubelgiji kifua mbele.
José Carlos Gonçalves Rodrigues, almaarufu kama Zeca alipatia timu yake
goli la kwanza katika dakika ya 73 lakini dakika ya 74 Lukaku akafungia
Ubelgiji bao la ushindi kwa kichwa.
Ubeligiji wanaongoza katika kundi H na alama 8 wakiwa bado na michezo
miwili ya kucheza.
Mashetani hao wekundu wamejiunga na Brazil, Iran na Japan katika kufuzu kwa
michuano ya Kombe la Dunia, huku Urusi wakijipatia nafasi ya moja kwa moja kwa
kuwa ni wenyeji wa michuano hiyo.
Bosnia-Herzegovina imeipita Ugiriki na kujipatia nafasi katika michezo ya
kufuzu kwa muondoano.
Hii ni baada ya Edin Dzeko kufunga magoli mawili yaliowapatia ushindi wa
magoli 4-0 huko Gibraltar na kujinyakulia nafasi ya pili katika kundi hilo
nyuma ya Ubelgiji.
- Syria yaweka hai matumaini kushiriki Kombe la Dunia
- Iran yafuzu kwa Kombe la Dunia 2018
- Italia imeichapa Liechtenstein bao 5-0 mechi ya kufuzu kombe la Dunia
Magoli mengine yalifungwa na Kenan Kodro na Senad Lulic upande wa vijana
hao wanaonolewa na Mehmed Bazdarevic ambao wako na alama 14, alama moja zaidi
ya Ugiriki.
Uswizi ilisalia na alama tatu mbele ya mabingwa wa Ulaya, Ureno baada ya
wote kupata ushindi siku ya Jumapili.
Goli la kujifunga la mlinda lango wa nyumbani Andris Vanins, bao la
mshambuliaji kutoka Blerim Dzemaili - ambaye hapo awali alikosa penalti - na
bao la kupitia penalti lake Ricardo Rodrigue, yaliwapatia timu hiyo ya Uswizi
ushindi huko Latvia.
Ureno ilijifaa baada ya Tamas Priskin kutolewa uwanjani na kupata ushindi
wa bao 1-0 kupitia Andre Silva huko Hungary
No comments: