Mourinho azua balaa Ulaya
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameonyesha umahiri wake wa kuwa
kipa baada ya kushiriki mechi ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia watu
walioathiriwa na moto wa jengo la Grenfell.
Mourinho alicheza kama kipa katika mechi hiyo Game4Grenfell kati ya timu
mbili za watu mashuhuri na wacheza soka wa zamani.
Fedha zilizopatika kutokana na tikiti za mechi hiyo zilienda katika mfuko
wa wale walioathiriwa na janga la moto.
Hata hivyo katika mechi hiyo, timu ambayo alikuwa akiichezea ilishindwa kwa
mabao 5-3 kwa njia ya penalty na bingwa wa olimpiki Mo Farah alifunga moja kati
ya mabao hayo.
Katika ajari hiyo ya moto watu 80 walifariki.
No comments: