Lwandamina arejea Yanga, aongoza mazoezi ya kuitungua Njombe Mji
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mzambia, George
Lwandamina tayari amerejea nchini akitokea kwao Zambia alipokuwa ameenda kwa
ajili ya kumzika baba yake mzazi aliyefariki dunia hivi karibuni.
Katika mazoezinya ya leo ya timu hiyo
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar Lwandamina ndiye
aliyekuwa akiongoza mazoezi hayo akisaidina na wasaidizi wake wa benchi la
ufundi tayari kwa kuwaweka fiti wachezaji wake kwa ajili ya mechi ijayo ya Ligi
Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji.
Yanga na Njombe Mji zitapambana na
Jumamosi ijayo katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
No comments: