Header Ads

Headline
recent

MAPEMA TU, TAYARI EPL IMEKULA KICHWA KIMOJA



LIGI KUU ya England maarufu kama EPL, kweli si ya mchezo kwani tayari imekula kichwa kimoja baada ya Klabu ya Crystal Palace, kutangaza kumfuta kazi kocha wa timu hiyo, Frank de Boer.
 
De Boer
De Boer ameshindwa kuiongoza vema Crystal Palace, kwani katika mechi nne za mwanzo za Ligi Kuu England msimu huu, timu hiyo haijapata pointi hata moja wala bao. Lakini timu hiyo ilishinda mechi moja pekee ya Kombe la Ligi dhidi ya Ipswich Town kwa matokeo ya 2-1.

Juni, mwaka huu, kocha huyo alisaini mkataba wa miaka mitatu klabuni hapo, lakini amedumu kwa siku 77 kabla ya kutimuliwa kwake.

Baada ya kocha huyo kutimuliwa, nafasi yake inachukuliwa na Roy Hodgson.
Hodgson

Ikumbukwe kuwa, De Boer anakuwa kocha wa tatu katika EPL kukaa siku chache kwenye timu tangu ajiunge nayo lakini anakuwa kocha wa kwanza kuongoza katika mechi chache kwenye ligi hiyo. Orodha kamili soma chini:

MAKOCHA WALIOKAA MUDA MFUPI KATIKA EPL
Les Reed (Charlton, 2006) – siku 40
Rene Meulensteen (Fulham, 2013-14) – siku 74
Frank de Boer (Crystal Palace, 2017) – siku 77
Bob Bradley (Swansea, 2016) – siku 84
Terry Connor (Wolves, 2012) – siku 91

MAKOCHA WALIOONGOZA KATIKA MECHI CHACHE EPL
Frank De Boer (Crystal Palace, 2017) – mechi 4
Les Reed (Charlton, 2006) – mechi 7
Bob Bradley (Swansea, 2016) – mechi 11
Jacques Santini (Tottenham, 2004) – mechi 11
Sammy Lee (Bolton, 2007) – mechi 11

MATOKEO YA DE BOER NDANI YA CRYSTAL PALACE
Agosti 12: v Huddersfield (walifungwa 3-0)
Agosti 19: v Liverpool (walifungwa 1-0)
Agosti 22: v Ipswich Town (walishinda 2-1) 
Agosti 26: v Swansea (walifungwa 2-0)
Sept 10: v Burnley (walifungwa 1-0)

No comments:

Powered by Blogger.