Manchester City VS Liverpool, Hatumwi Mtoto Dukani
Manchester City na
Liverpool wataingia dimbani Etihad mapema Jumamosi katika mbio za
kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza
Timu zote mbili zimo ndani ya nne bora za kwenye msimamo wa Ligi
zikiwa zimejikusanyia alama saba kutoka kwenye mechi zao tatu za
mwanzo, ingawa City bado hawajashinda mechi ya nyumbani kwani
walilazimishwa sare ya 1-1 na Everton.Kwa upande wa Liverpool, wameshinda mechi zote za nyumbani - ikiwa ni pamoja na kipigo cha 4-0 walichoipa Arsenal - lakini walipata sare pekee ya 3-3 dhidi ya Watford mechi ya ufunguzi.
No comments: