Header Ads

Headline
recent

AZAM: Simba Lazima Wachezee Kichapo



Azam wakicheza kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wao wa nyumbani wamepania kuifanyia kitu kibaya Simba
Miamba ya soka Tanzania Azam na Simba, kesho zinakutana katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambao utapigwa uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Mpambano huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na timu hizo kubadilishana wachezaji hasa Simba ambayo inawachezaji wanne waliotokea  kikosi cha Azam.
Pambano hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa 10:00 badala ya 1 usiku kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Kocha wa Azam FC, Mromania Aristica Cioaba,  ameimabia Goal kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya pambano hilo la kesho.
Cioaba amesema anakwenda kwenye mchezo huo akiwa anajivunia utarari wa kikosi chake ambacho kinaundwa na wachezaji wengi vijana wenye uwezo mkubwa wa kucheza soka kwa kufuata maelekezo yake.
“Nimchezo mzuri kwasababu tunacheza na timu kubwa Tanzania lakini tumejianda kuonyesha uwezo wetu na kuwashangaza wale wote ambao wamekuwa wakitubeza kutokana na kuondoka kwa baadhi ya wachezaji nyota,”amesema Cioaba.
Kocha huyo anayependa kutumia mfumo wa 4-3-3, amesema katika mchezo huo atawatehemea zaidi wachezaji wake wazoefu kama kipa Mwadini Ally, Himid Mao, Salum Abubakari na wachezaji raia wa Ghana Yahya Mohamed na Yakubu Mohamed ambao anaamini watafanya vizuri na kumpatia ushindi wa pili mfululizo kwenye ligi hiyo.
Kwaupande wake kocha wa Simba Joseph Omog, amesema huo ni mchezo mwepesi kuliko ule ambao waliibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani wiki moja na nusu iliyopita.
Omog amesema anajivunia uwepo wa nyota wake wote ambao amewasajili msimu huu na anaamini ushindi kwa kikosi chake kesho ni lazima.
“Asilimia kubwa ya wachezaji wangu na hata mimi mwenye tunaujua vizuri uwanja wa Azam Complex kwahiyo siyo kikwazo ambacho kitatufanya tushindwe kupata matokeo katika mchezo huo ambao tumedhamiria kufanya maajabu kama yale tuliyoyaonyesha kwenye mchezo wa kwanza,”amesema Omog.
Kocha huyo amesema kama ilivyo kawaida yake atatumia mfumo wa 4-4-2 huku akimwanzisha kikosi cha kwanza mshambuliaji Nicholaus Gyan ambaye aliukosa mchezo wa kwanza dhidi ya Ruvu Shooting.
Kocha huyo amesema amepania kuhakikisha msimu huu hapotezi pointi hata moja mbele ya timu kubwa za Azam na Simba na hilo atalidhihirisha kwenye mpambano huo ambao wamejipanga kuzima kelele za wapinzani wao.
Katika mchezo huo wachezaji wanne wa Simba Shomari Kapombe, Aishi Manula,Erasto Nyoni na John Bocco watarudi kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Chamaz Complex baada ya kuachana na timu hiyo baada ya mikataba yao kumalizika.
Azam pia inajivunia washambuliaji Mbaraka Yusufu na Waziri Junoir ambao imewasajili msimu huu kutoka Kagera Sugar ambao watashirikina na wachezaji waliopo.


No comments:

Powered by Blogger.