Header Ads

Headline
recent

BUSWITA: Nitawafurahisha Mashabiki Wangu wa Yanga.


Baada ya kutoka jela ya soka kwa kuruhusiwa kuichezea Yanga mshambuliji wa Yanga Pius Buswita atamba kuifanyia makubwa Yanga
Mshambuliaji wa Yanga Pius Buswita, amesema atahakikisha analipa fadhila kwa kuifungia timu yake mabao katika mechi mbili wanazokwenda kucheza kwenye miji ya Njombe na Songea.
Buswita amesema, yupo fiti kuhakikisha anafanya kila liwezekanalo ili kuipa ushindi na hilo litawezekana kutokana na sapoti kubwa anayoipata kutoka kwa uongozi wa timu hiyo.
“Nashukuru kwa uongozi wa Yanga kunipigania hadi kupata nafasi hii ya kucheza baada ya awali kufungiwa kwa mwaka mmoja,”amesema Buswita.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Mbao amesema anajutia kosa hilo na kamwe hatorudia tena kutokana na kujifunza yaliyotokea.
Amesema amejifunza mengi na amewaomba radhi uongozi wa TFF, na klabu ambayo alitokea ya Mbao FC.



No comments:

Powered by Blogger.