Azam FC kumalizana na Kagera Sugar kesho, Simba, Yanga nazo mzingoni Jumamosi
Mzunguko wa
Tatu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea mwishoni
mwa wiki hii.
Kwa mujibu
wa ratiba ya VPL, kesho Ijumaa Septemba 15, 2017 Azam FC itaialika Kagera
Sugar saa 1.00 usiku (19h00) katika Uwanja wa Azam ulioko Chamazi jijini Dar es
salaam.
Kwa siku ya
Jumamosi Septemba 16, 2017 Majimaji FC ya Songea itacheza na Young
Africans ya Dar es Salaam, saa 10.00 jioni (16h00) katika Uwanja wa Majimaji
mkoani Ruvuma.
Mbao
itasafiri hadi Manungu mkoani Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo
ambao pia utapigwa Jumamosi saa 16h00 wakati Tanzania Prisons ya Mbeya itakuwa
mwenyeji wa Ndanda FC saa 16h00 kwenye Uwanja wa Sokoine.
Lipuli Fc itakuwa
mwenyeji wa Ruvu Shooting saa 16h00 katika Uwanja wa Samora, Iringa wakati
Stand United itacheza na Singida United saa 16h00 kwenye Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga.
No comments: