TFF yawaonya wasiozingatia utaraibu wa mawasiliano
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), lingependa kutoa maelekezo ya kufuatwa kwa
utaratibu wa mawasiliano kwa mfumo wa halakia yaani ngazi moja baada ya
nyingine kwa ukubwa.
Mawasiliano
hayo yanalenga zaidi katika kualika viongozi wa kitaifa wa TFF katika programu
au shughuli mbalimbali za maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.
TFF
ingependa kuelekeza kuwa kama kuna suala la mwaliko au barua ya kwenda viongozi
wa juu kuanzia kwa wadau, ngazi ya wilaya na mkoa kupita hatua moja baada ya
nyingine kabla ya kufika katika ofisi ya Katibu Mkuu.
Tungependa
kwa pamoja tushirikiane kwa kuheshimu mamlaka za mpira wa miguu zilizoko kwenye
maeneo husika badala ya kufanya mawasiliano ya moja kwa moja na viongozi juu.
No comments: