Ligi Daraja la Kwanza kuanza Jumamosi
Ligi Daraja
la Kwanza (FDL) inatarajiwa kuanza Jumamosi Septemba 16, 2017 katika viwanja
vinne tofauti nchini kwa mujbu wa ratiba iliyotoka mwezi uliopita.
Kwa mujibu
wa Ratiba ya FDL, katika Kundi A: Mgambo itacheza na JKT Ruvu katika Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga wakati Kundi B: kutakuwa na michezo miwili.
Michezo hiyo
miwili itakuwa ni kati ya Mawenzi Market itakayokuwa mwenyeji wa KMC ya
Kinondoni, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Mufindi United
itakuwa mgeni wa Polisi Dar kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es
Salaam.
Kundi C:
kutakuwa na mchezo mmoja kwa siku ya Jumamosi ambako Rhino ya Tabora itakuwa
mwenyeji wa Alliance Schools kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Ni ligi ya
mabadiliko: Ligi ya msimu huu ina mabadiliko makubwa mawili yaliyopitishwa na
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kwanza ni
kupandisha idadi ya timu zitakazopanda daraja badala ya tatu (moja kutoka
katika kila kundi) hadi timu sita (timu mbili kutoka katika kila kundi)
zitakazocheza Ligi Kuu msimu ujao wa 2018/19.
Ligi Kuu
msimu ujao itakuwa na timu 20 kutoka timu 16 zinazoshiriki kwa sasa.
Kwa mujibu
wa mabadiliko hayo, VPL msimu huu itashusha timu mbili tu na kubaki 14 ambazo
zitasubiri sita zitakazopanda daraja.
Mabadiliko
mengine yanahusu Kanuni ya 25 ambako sasa mara baada ya makato ya msingi katika
mapato ya mlangoni, asilimia 60 itakwenda kwa timu mwenyeji badala ya kugawanywa
kama ilivyokuwa awali.
Hii italeta
juhudi kwa timu mwenyeji kuitangaza timu yake na mchezo wake kwa wadau wengi
ili ivue mapato makubwa tofauti na miaka iliyopita ambako TFF imeona kwamba
kulikuwa na kutegeana kutangaza mechi.
Makundi ya
Daraja, kundi ‘A’ lina timu za African Lyon, Ashanti United, Friends Rangers na
Mshikamano za Dar es Salaam wakati nyingine ni JKT Ruvu na Kiluvya United za
Pwani, Mgambo JKT ya Tanga na Mvuvumwa ya Kigoma.
Kundi ‘B’
ziko za Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam,
Mawezi Market NA Polisi Tanzania za Morogoro, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi
United ya Iringa na Polisi Dar Ya Dar es Salaam.
Kundi ‘C’
lina timu za Alliance School, Pamba na Toto
African za
Mwanza, Rhino Rangers ya Tabora, Bishara Mara ya Mara, Dodoma FC ya
Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.
No comments: