TFF yatoa onyo kali kwa klabu za ligi kuu
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa muda kwamba hadi Septemba 22, klabu
zote 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na za zile 24 Ligi
Daraja la Kwanza (FDL), ziwe zimekamilisha taratibu za kupata Leseni za Klabu.
Kwa mujibu
wa Kamati ya Leseni za Klabu, ni timu tano za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
kati ya 16 hazikuchukua hata fomu za maombi ya Leseni za klabu wakati Klabu 11
zimebainika kuwa na upungufu mkubwa katika kukamilisha vigezo.
Kamati ya
Leseni za Klabu imekutana zaidi ya mara tatu katika vikao na kujiridhisha
kwamba kwa ujumla vigezo vifuatavyo havijakamilika kwa asilimia 100 katika
klabu nyingi kama zifuatavyo.
1. Klabu
zote hazina programu ya kuendeleza mpira kwa vijana.
2. Taarifa
za klabu haielezi kuhusu miundombinu ya kuhudumia walemavu wakati wa mchezo.
3. Klabu
hazijaonesha uwanja wa mazoezi.
4.
Hazijaambatanisha mikataba ya watendaji kama vile Katibu Mkuu; Ofisa Usalama wa
timu, Mhasibu au mkurugenzi wa fedha, na daktari n.k.
5. Taarifa
hazina maelezo ya kocha wa timu za vijana.
6. Klabu
hazijajaza fomu za kuomba Leseni ya klabu.
7.
Hazijambatanisha katiba ya klabu.
8. Klabu
hazijaambatanisha ripoti ya fedha ya mwaka.
9. Klabu
hazijajaza fomu ya kuthibitisha kushiriki mashindano ya Ligi Kuu ya Vodacom.
Kwa taarifa hii kwa umma, Kamati ya Leseni ya Klabu inazitaka klabu kukamilisha vigezo hivyo kabla ya Septemba 22, mwaka huu. Vinginevyo, klabu inaweza kuondolewa kwenye mashindano.
No comments: