Yanga yaipiga mkwara Bodi ya Ligi
Uongozi
wa klabu ya Yanga umeitaka Bodi ya Ligi Tanzania (TPBL), pamoja na Kampuni ya
Vodacom Tanzania kuiandikia barua klabu hiyo ya kuiomba radhi klabu hiyo kwa
kitendo kilichojitokeza juzi Alhamisi katika hafla ya kukabidhi vifaa vya
michezo kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara.
Katika
hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Yanga haikuwakilishwa na kiongozi
wake yeyote kutokana na kilie kilichodaiwa kuwa haikupewa taarifa za kuwepo kwa
tukio hilo na badala yake Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu ya
Simba ambayo ni mahasimu wao kubwa, Haji Mara aliamua kujitolea kuwawakilisha
watani zao hao wa jadi.
Kitendo
hicho cha Manara kuiwakilisha Yanga katika hafla hiyo kimewakera vilivyo viongozi
wa Yanga na kuona kama vile klabu yao hiyo imedhalilishwa na kushushwa hadhi
yake iliyonayo katika soka la Tanzania ukilinganisha na timu nyingine zote
zinazoshiriki ligi kuu ikiwemo Simba.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari leo, Katibu Mkuu
wa Yanga, Charles Mkwasa alisema kuwa kutokana na hali hiyo, uongozi wa Bodi ya
Ligi pamoja na Vodacom wanatakiwa
kuiomba klabu hiyo.
Alisema
endapo watashindwa kufanya hivyo basi, watalazimika kuchukua hatua kali ikiwa
ni pamoja na kwenda mahakamani kuishitaki Bodi ya Ligi pamoja na Vodacom kwa
kitendo chao cha kumuruhusu Manara kuwakirisha Yanga katika zoezi hilo pasipo
kuwasiliana na uongozi wa klabu hiyo.
“Jambo
hilo kusema kweli lilitusikitisha sana kwani limetudhalilisha sana na limevunja
hadhi ya klabu ya klabu yetu ambayo tumeitafuta kwa muda mrefu ukilinganisha na
timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu.
“Tunawaomba
wa Bodi ya Ligi na Vodacom kutuandikia barua ya kutuomba radhi kwa hilo lakini
pia kutusafisha kwa kashifa waliyoieneza kuwa tulishindwa kutokea katika hafla
hiyo wakati hatukupewa taarifa yoyote ile juu ya kufanyika kwa hafla hiyo, kama
watashindwa kufanya hivyo nadi tutachukua hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kwenda
mahakamani kutokana na udhalilishwaji huo,” alisema Mkwasa.
No comments: