Vodacom Yagawa Vifaa Kwa Timu za Ligi Kuu
Kampuni ya
mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom leo imegawa vifaa kwa
timu 16
zitakazoshiriki ligi kuu msimu huu wa 2017/2018.
Vifaa hivyo ni jezi,
sare za mazoezi, viatu, mabegi, trakisuti, soksi, vilinda ugoko na
sare za waamuzi.
Mkurugenzi wa idara
ya masoko wa Vodacom, Hisham Hendi alisema kuwa kampuni
yake imejipanga
kuhakikisha mchezo wa soka unapiga hatua nchini.
"Kuelekea msimu
ujao Vodacom imejipanga kufanya mambo makubwa zaidi kwenye
ligi tukiamini
mchezo wa soka unaunganisha watu lakini pia ni ajira.
Tumewaandalia mambo
mazuri mashabiki wa soka ambao wengi ni wateja wetu,"
alisema Hendi.
Mkurugenzi mtendaji
wa bodi ya Ligi Kuu, Boniface Wambura alisema kuwa
watahakikisha
wanatatua changamoto zilizojitokeza msimu uliopita.
"Changamoto
kubwa ilikuwa ni waamuzi, lakini tayari tumeshakutana na kamati ya
waamuzi ili
kuhakikisha tunapata waamuzi watakaokidhi viwango," alisema
Wambura.
Ofisa habari wa
Simba, Haji Manara akizungumza kwa niaba ya klabu, alitoa wito
kwa bodi ya ligi
kutobadilisha ratiba.
Hii inaziumiza timu
ambazo hazina uwezo wa kifedha na kufanya ligi kupoteza
ushindani. "alisema
Manara".
No comments: