MVUA YA MABAO 'YANYESHA' USIKU WA ULAYA LEO
LIGI ya Mabingwa Ulaya, imeendelea usiku wa Oktoba 17, mwaka
huu ikiwa ni hatua ya makundi ambapo zilipigwa mechi nane za Kundi E, F, G na H
huku ikishuhudiwa mvua ya mabao kwa baadhi ya meci hizo.
Maribor vs Liverpool |
Katika Kundi E, Liverpool ikiwa ugenini, iliibuka na ushindi
mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Maribor, huku Spartak Moscow ikiichapa nyumbani
Sevila kwa mabao 5-1.
Man City vs Napoli |
Feyenoord iliyopo Kundi F, imekubali kichapo cha mabao 2 – 1 kutoka
kwa Shakhtar Donetsk, huku Manchester City ikiichapa Napoli mabao 2 – 1.
RB Leipzig vs Porto |
Monaco ikiwa nyumbani, imechapwa 2-1 na Besiktas, wakati RB
Leipzig ikiinyuka Porto mabao 3 – 2. Hilo ni Kundi G.
Madrid vs Tottenham |
Kwenye Kundi H, mechi
zote ziliisha kwa sare ambapo matokeo yake yalikuwa hivi; APOEL Nicosia 1 – 1 Borussia
Dortmund na Real Madrid 1 – 1 Tottenham Hotspur.
No comments: