Header Ads

Headline
recent

OKWI ALIVYOIBEBA SIMBA



EMMANUEL Arnold Okwi, Oktoba 15, 2017 aliifungia timu yake bao dakika ya 90 na kuambulia pointi moja baada ya sare ya 1-1 mbele ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Okwi (kulia)

Sare hiyo imeifanya Simba kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 12 sawa na Mtibwa Sugar, Yanga na Azam FC baada ya zote kucheza mechi sita.
Mtibwa Sugar ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa straika wake, Stamili Mbonde aliyefunga kwa kichwa akiunganisha kona iliyochongwa na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ dakika ya 36.
Wakati wengi wakiamini kwamba Mtibwa itaondoka na pointi zote tatu, Okwi alifunga bao la kusawazisha ikiwa ni ndani ya dakika tatu za nyongeza kwa njia ya faulo ya moja kwa moja akiwa nje kidogo ya eneo la hatari la Mtibwa.
Kikosi cha Simba
Kikosi cha Simba kilikuwa hivi; Aishi Manula, Ally Shomari, Erasto Nyoni, Salim Mbonde/Juuko Murshid dk46, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Said Ndemla dk63, James Kotei, John Bocco/Juma Liuzio dk16, Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima.
Kikosi cha Mtibwa
Mtibwa Sugar; Benedict Tinoco, Salum Kanoni, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Dickson Daud, Cassian Ponera, Shaaban Nditi, Salum Kihimbwa/Henry Joseph dk90, Mohamed Issa, Stamili Mbonde/Kevin Sabato dk57, Salum Khamis/Hassan Dilunga dk69 na Ally Makarani.

No comments:

Powered by Blogger.