Zullu apigwa chini rasmi Yanga
Wakati dirisha la usajili kwa timu za Ligi Kuu Bara likitarajiwa kufungwa kesho
Jumapili, Agosti 6, uongozi wa Yanga jana umetangaza rasmi kuachana na kiungo
wake wa kimataifa raia wa Zambia, Justine
Zullu.
Yanga imefikia hatua hiyo baada ya kutolizishwa na kiwango cha mchezaji huyo aliyejiunga na timu hiyo msimu uliopita katika dirisha dogo la usajili akitokea Zesco FC ya Zambaia kwa ajili ya kuimarisha safu yake ya kiungo mkabaji ambayo imekuwa ikiitesa kwa muda mrefu.
Hata
hivyo, mara baada ya kujiunga na timu hiyo Zullu, alishindwa kuonyesha ubora
wake uwanjani kama Yanga walivyotarajia kuuona kutoka kwake.
Katibu
Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema kuwa kutokana na hali hiyo wameamua
kuachana na mchezaji huyo na nafasi yake itachukuliwa mchezaji mwingine ambaye muda
wowote kuanzia leo watamtangaza kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili hiyo
kesho.
“Ni
kweli kabisa tumeamua kuachana na Zullu kutokana kutolizishwa na kiwango chake
uwanjani kwani hakikuwa kama tulivyotajia.
“Kwa
kuwa mtazamo wa klabu yetu ni kuona tunafika mbali imetubidi tufikia hatua hiyo
na hivi karibuni tulizungumza na wakala wake na tumefikia makubaliano kwa hiyo
hivi sasa tunachofanya ni kumalizana naye bila ya kufikishana Fifa (Shirikisho
la Soka la Kimataifa),” alisema Mkwasa.
No comments: