Tegete asaini mwaka mmoja majimaji FC
TIMU
ya soka ya Majimaji imefanikiwa
kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Yanga na timu ya Mwadui, Jerson Tegete.
Majimaji
imesajili Tegete kwa mkataba wa mwaka mmoja ili aweze kuiongezea nguvu safu
yake ya ushambuliaji katika michuano ya Ligi Kuu Bara msimu ujao inayotarajia
kuanza kutimua vumbi Agosti 26, mwaka huu.
Tegete
amesema kuwa amefikia uamuzi huo wa kujiunga na Majimaji kwa lengo la kutaka
kurudisha makali yake aliyokuwa nayo hapo zamani.
“Nimesaini
mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Majimaji, hata hivyo nimefikia uamuzi huo
ili niweze kuitumia timu hiyo kurudisha kiwango changu nilichokuwa nacho hapo
zamani.
No comments: