Nemanja Matic Rasmi Manchester United Kwa £40m.
Nemanja Matic Akisaini Kandarasi Mpya Mu |
Matic pindi alipokuwa Manchester United |
Matic Akiwa kwenye harakati uwanjani |
Manchester United wamekamilisha ununuzi wa kiungo wa kati wa Serbia Nemanja Matic kutoka kwa mabingwa wa Ligi ya Premia Chelsea kwa £40m.
Mchezaji huyo ametia saini mkataba wa miaka mitatu.
Matic, 28, amekuwa mchezaji wa tatu kununuliwa na United majira haya ya joto.
United walikuwa wamemnunua beki Victor Lindelof kwa £31m kutoka Benfica na kisha wakalipa £75m kumchukua Romelu Lukaku kutoka Everton.
Meneja wa United Jose Mourinho alimweleza Matic kama mchezaji anayecheza vyema na wenzake kwenye timu na "ana kila kitu ambacho tungetaka katika mwanakandanda; uaminifu, uendelevu na kuwa na ndoto kuu".
Matic amesema ana furaha sana kujiunga na United wakati huu wa kusisimua.
Mourinho, alipokuwa Chelsea, alitumia £21m kumnunua Matic kutoka Benfica kwa kipindi cha pili Stamford Bridge Januari 2014.
Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Nemanja Matic aliachwa nje ya kikosi cha Chelsea kilichosafiri bara Asia kujiandaa kwa msimu ujao
Thamani yake ilikuwa imekadiriwa kuwa chini ya £5m alipoihama klabu hiyo kama kikolezo wakati wa ununuzi wa David Luiz Januari 2011, miaka miwili baada yake kujiunga na Blues kwa mara ya kwanza kwa £1.5m kutoka kwa klabu ya MFK Kosice ya Slovakia.
Matic alifunga bao moja katika mechi 35 alizochezea Chelsea Ligi ya Premia msimu wa 2016-17, ambapo pia alifunga bao la kipekee wakati wa ushindi wao nusufainali Kombe la FA dhidi ya Tottenham Aprili.
No comments: