Erasto Nyoni aibeba Simba Sauzi akitoka sare na Bidvest
TIMU
ya Simba imecheza mechi yake ya pili ya kirafiki dhidi ya Bidvest ya Afrika
Kusini na kufanikiwa kutoka sare ya bao 1-1.
Mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa imeinyuka leo
hii asubuhi katika Uwanja wa Sturrock Park jijini Johannesburg.
Katika
mechi hiyo, Simba ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika 33 kupitia
mchezaji wake mpya, Erasto Nyoni.
Hata
hivyo Bidvest walisawazisha bao hilo katika kipindi cha pili cha mchezo huo dakika
ya 70.
Mechi
hiyo ilikuwa ni ya pili kwa Simba tangu ilitua kwa ajili ya kambi yake ya kujiandaa
na ligi kuu msimu ujoa, ambapo mechi ya kwanza ilifungwa bao 1-0 na Orlando
Pirates.
No comments: