Omog atua Yanga kumfuata Ajibu
Bada ya hivi
karibuni, mshambuliaji mpya wa Yanga, Ibrahimu Ajibu kushindwa kuiongeza timu
hiyo kuibuka na ushindi dhidi ya Lipuli FC, kocha wake wa zamani Mcameroon,
Joseph Omog inadaiwa kuwa anajipanga ili aweze kutua Yanga kwa ajili kufanya
naye mazungumzo mafupi.
Omog ambaye ni
Kocha Mkuu wa Simba na aliyekuwa akimufundisha Ajibu msimu uliopita kabla ya
kujiunga na Yanga inadaiwa kuwa anataka kukutana na Ajibu ili aweze kuzungumza
naye juu ya nini anachopaswa kufanya kama anataka kufanya vizuri msimu huu.
Inadaiwa kuwa Omog
amefikia uamuzi huo kwa kuwa ni shabiki mkubwa Ajibu kutokana na kipaji chake na
amekuwa hapendi kuona kikipotea.
Habari za
kuaminika kutoka ndani ya Simba ambazo zimedai kuwa jambo kubwa ambalo Omog
anatarajia kumwambia Ajibu mara tu atakapoonana naye ni kuhusiana na kubadili
mfumo wake wa maisha.
“Amejaribu
kumtafuta mara kadhaa kwa njia ya Simu lakini hajampata ila jambo kubwa
analotaka kumwambia endapo atafanikiwa kuonana naye siku yoyote ni juu ya kubadili mfumo wake wa maisha kama
kweli anataka kufanikiwa.
“Mara nyingi
alikuwa hafurahishwi na jinsi Ajibu alivyokuwa anaishi wakati alipokuwa Simba
licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza soka, kwa hiyo hivi sasa anataka
kumuona akiachana na maisha hayo na akili yake aweze kuilekeza zaidi mazoezini
na kuzingatia yale yote anayoambiwa viongozi wake wa ufundi,” kilisema chanzo
hicho cha habari.
Hata hivyo
alipolizwa Omog kuhusiana na hilo alisema kuwa: “Siyo kwamba nataka kufuata
Yanga ila nikipata bahati ya kukutana naye nitamshauri kuhusiana na hayo.
“Ajibu ni mmoja
kati ya wachezaji wachache hapa nchini wenye vipaji vya juu hivyo siyo jambo
zuri kumuacha akapotea, binafsi ni shabiki wake mkubwa na siku zote nimekuwa
nikitaka kumuona afike mbali na ikiwezekana awe kama Mbwana Samatta.
“Ana kipaji cha
hali ya juu hivyo ni kitendo cha yeye sasa kubadilika na kutamani zaidi
mafanikio,” alisema Omog.
No comments: