Header Ads

Headline
recent

Njombe waitisha Yanga



Kacho Mkuu wa Njombe Mji, Hassan Banyai amesema kuwa anataka kuandika rekodi ya pekee katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaoikutanisha timu hiyo dhidi ya Yanga itakayofanyika Jumatano ijayo.

Mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa utafanyika katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

Banyai asema kuwa ana hamu kubwa sana ya kuona timu yake hiyo ikiitandika Yanga mabao mengi katika mchezo huo kwa mara ya kwanza baada ya kutinga ligi kuu msimu huu.

Alisema kitendo hicho kitaipatia heshima kubwa timu yake hiyo na kuiwezesha kufuatiliwa kwa kalibu na wapenzi pamoja na mashabiki wa soka hapa nchi jambo ambalo litaisaidia katika kujiimarisha kiuchumi.

“Msimu uliopita Mbao ya Mwanza ilifanikiwa kuzigomea Yanga na Simba jambo ambalo liliwafanya watu wengi kuifuatilia na hivi karibuni inafanikiwa kupata udhamini wa mamilioni ya fedha.

“Kwa hiyo na mimi nataka niandike rekodi ya pekee kwa kuifunga Yanga mabao Mengi ili na sisi tupate kufuatiliwa na watu wengi jambo ambalo litatusaidia pia kupata wadhamini na mwisho wa siku tukajiimarisha kiuchumi,” anasema Banyai.

Kuhusu maandalizi ya mechi hiyo, Banyai alisema kuwa; “Tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika mechi hiyo ili tuweze kulipa kisasi cha kupoteza mechi yetu ya kwanza msimu huu dhidi ya Prisons ambayo tulifungwa mabao 2-1.”

No comments:

Powered by Blogger.