Okwi aiwahi Azam FC
Wachezaji wawili wa Simba, Waganda, Juuko Murshid na mshambuliaji,
Emannuel Okwi waliokuwa na kikosi cha timu ya taifa ya Uganda wanatarajiwa
kuwasili nchini leo kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Azam.
Simba SC itacheza na Azam Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jiji Dar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Manara amesema kuwa,
Juuko na Okwi watafika leo na moja kwa moja wataungana na wenzao kwa ajili ya
maandalizi ya mechi hiyo.
No comments: