Kuwaona Azam na Simba ni Buku Kumi
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji Azam dhidi ya Simba unaotarajiwa kupigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Azam FC |
Mchezo huo ambao utapigwa kuanzia saa 1 kamili usiku, viingilio vyake vimegawanywa makundi mawili. Kundi la kwanza ni la V.I.P ambapo sehemu hiyo ina uwezo wa kuchukua watu 1000. Katika sehemu hiyo, kiingilio ni Sh 10,000.
Baadhi ya wachezaji wa Simba wakijiweka fiti dhidi ya mchezo huo |
Kundi la pili ni lile jukwaa la mzunguko lenye uwezo wa kuchukua watu 6000. Sehemu hiyo kiingilio chake ni Sh 7000.
No comments: