Kipa kiboko ya Simba afariki dunia
SHIRIKISHO
la Soka la Rwanda, (Ferwara), limethibitisha kuwa, mlinda mlango wa zamani wa Sofapaka
na timu ya taifa ya Rwanda, Evariste Mutuyimana, amefariki dunia leo Jumanne
akiwa nyumbani kwake, Kigali, Rwanda.
Mlinda
mlango huyo amefariki akiwa na miaka 26 ambapo alikuwa akiitumikia Klabu ya Rayon
Sports ya Rwanda kabla ya kufikwa na mauti hayo huku chanzo cha kifo chake kikitajwa
kuwa ni tatizo la kushindwa kupumua vizuri kutokana na matatizo ya moyo
yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
“Mutuyimana
alikuwa na matatizo ya moyo kwa muda mrefu sasa. Kwa bahati mbaya tumempoteza. Alikuwa
mlinzi mzuri na Rwanda kwa kweli imempoteza mtu muhimu,” alisema Ofisa Habari
wa Ferwara, Bonnie Mugabe.
Juni,
mwaka jana, Mutuyimana alijiunga na Rayon Sports inayoshiriki Ligi Kuu ya
Rwanda maarufu kama Azam Rwanda Premier League baada ya kukaa kwa kipindi cha
miezi 18 katika kikosi cha Sofapaka inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya maarufu kama
SportPesa Premier League (SPL).
Mlinda
mlango huyo, atakumbwa na Watanzania kutokana na miezi michache iliyopita timu
yake ilipocheza dhidi ya Simba katika mchezo wa Tamasha la Simba Day na
kufungwa bao 1-0, yeye alikaa langoni dakika zote tisini. Mechi hiyo ilipigwa
Agosti 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
No comments: