Sauzi wakubali mechi yao na Senegal kurudiwa
Viongozi wa ngazi ya juu katika
Shirikisho la Soka Afrika Kusini (Safa) wamekubali mechi yao ya kuwania kufuzu
kushiriki Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 ambapo Afrika Kusini iliibuka
mshindi dhidi ya Senegal inastahili kurudiwa.
Shirikisho la soka la Kimataifa FIFA
limetoa ilani kwamba mechi hiyo irudiwe baada ya mwamuzi aliyechezesha mechi
hiyo, Joseph Lamptey kupigwa marufuku kwa kutoisimamia vyema mechi hiyo.
Safa imekuwa ikitathmini jinsi ya
kukata rufaa lakini kwa sasa imesema imekubaliana na Fifa.
Hata hivyo shirikisho hilo limesema
lingekata rufaa iwapo mashtaka ya mwamuzi huyo yangebatilishwa.
Afrika Kusini iliichapa Senegal
magoli 2-1 katika
mechi waliotoka sare mwaka jana.
No comments: