Kadi nyekundu leo inakuchambulia wachezaji kadhaa wenye deni kubwa kwa msimu ujao kwenye timu zao
Pazia la Ligi Kuu linatarajiwa kufunguliwa rasmi Agosti 26 kwa
klabu zote 16 kuanza kuzisaka alama, bingwa mtetezi Yanga atafungua
dimba na Lipuli huku Simba wakiikaribisha klabu ya RUVU Shooting
katika uwanja wa Taifa
Kadi nyekundu inakuchambulia
wachezaji kadhaa wenye deni kubwa kwa msimu ujao kutokana na
matarajio makubwa waliyonao mashabiki dhidi ya ya nyota hao,
matarajio hayo makubwa yanatokana na gharama kubwa zilizotumika
kwenye usajili wao na historia zao za kuvutia katika klabu walizotoka
Ibrahim Ajibu (Yanga)
|
Ibrahim Ajibu (Yanga) |
Ana kazi kubwa wa kuonesha ubora wake ndani ya Yanga kama ule
aliokuwa nao Simba kwa msimu ya nyuma, licha ya presha iliyopo nyuma
yake ila mashabiki wa Jangwani wanasubiri kumuona Ajibu akifanya kazi
kubwa mara mbili na alipotoka
Emmanuel Okwi (Simba)
|
Emmanuel Okwi (Simba) |
Ni mchezaji mwenye rekodi nzuri katika soka la ukanda huu wa
Afrika Mashariki, historia yake ya huko nyuma ndiyo changamoto kubwa
sana kwake, mashabiki wengi wanatarajia wakimuuona nyota huyo
akianzia pale alipoishia miaka mitatu nyuma na siyo tofauti na hivyo,
Okwi ana deni kubwa la kufanya ili kuwashawishi mashabiki
Haruna Niyonzima (Simba)
|
Haruna Niyonzima (Simba) |
Ndiye mchezaji anayesubiriwa kwa hamu kubwa msimu ujao kutokana na
usajili wake kuwa na sinema nyingi, kutokana na gharama kubwa za
kuipata saini yake yake Wanamsimbazi hawatataka kusikia zaidi ya
kiwango bora kwake tu
Danny Usengimana (Singida United)
|
Danny Usengimana (Singida United) |
Mrwanda huyo ndiye mchezaji ghali kuliko wote katika klabu yake ya
Singida United, mtihani uliopo mbele yake ni kuthibitisha ubora wake
kwamba unaendana na gharama zilizotumika kwenye usajili wake
Juma Nyosso (Kagera Sugar)
|
Juma Nyosso (Kagera Sugar) |
Hakuwa kwenye Ligi kwa muda wa miaka miwili kutokana na adhabu ya
kufungiwa na TFF kutokana na utovu wa nidhamu, Nyosso amemaliza
kifungo chake hivyo ni ruksa kucheza kwa msimu ujao, kitendo cha
Kagera kumwamini na kumpa nafasi ni kama deni kubwa kwa beki
huyo kwa sasa anaitaji kufanya kazi kubwa ili kuweza kurudisha
fadhira ndani ya klabu kwa kumpa nafasi
No comments: