Header Ads

Headline
recent

Madrid Yairarua Barcelona 3-1


Real Madrid jana Usiku imeifunga Barcelona magoli 3-1 katika mechi ya kwanza ya kombe la supacopa de Espana kwenye uwanja wa Camp Nou.
Magoli ya Real Madrid yalifungwa na Cristiano Ronaldo kwenye dakika ya 80, Marco Asensio dakika ya 90 na goli la tatu alijifunga mwenyewe beki wa Barcelona, Gerard Pique dakika 50.
Goli pekee la Kufutia machozi lilifungwa na Lionel Messi kwa njia ya penatiti baada ya Keylor Navas kumuangusha Luis Surez kwenye Eneo la hatari katika dakika 77.
Katika mchezo huo tulishuhudia Cristiano Ronaldo akionesha kiwango kizuri cha mchezo licha ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu aliyoipata baada ya kupata kadi mbili za njano dakika 82.

ANGALIA MAGOLI YALIVYOFUNGWA HAPA

No comments:

Powered by Blogger.