Lwandamina azushiwa kutimuliwa Yanga
SIKU moja baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii, kuliibuka
taarifa kuwa Kocha wa Yanga, George Lwandamina alikatiwa tiketi ya ndege ya
kuondoka Dar kwenda kwao Zambia.
Hata hivyo Lwandamina amekanusha madai hayo na kudai
kuwa hayana ukweli wowote.
Taarifa za awali zilianza kusambaa baada ya kuonekana
nakala ya tiketi ya Kampuni ya Fastjet ikionyesha kocha huyo anatarajia
kuondoka leo Ijumaa saa 4:50 usiku kuelekea Zambia ambapo angefika kesho
Jumamosi saa 6:20 usiku.
Tiketi hiyo ambayo inaonyesha namba ya ndege ambayo ni
FN0250, inaonyesha jina la kocha huyo ambaye ndiyo msafiri na malipo yake
yalitakiwa kufanywa jana Alhamisi kabla ya safari hiyo.
Uongozi wa Yanga ulikanusha taarifa hizo na
alipotafutwa Lwandamina mwenyewe alisema: “Watu wengine huongea kwa niaba
yangu.” Alipotumiwa nakala ya tiketi akajibu: “Hiyo ni tiketi bandia.”
No comments: