Fifa yaitumia salamu za pongezi TFF
Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino, ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa TFF kwa kipindi cha miaka minne ijayo ya 2017-2021.
Rais Infantino katika barua yake ya Agosti 14, 2017 aliyoiandika
kutoka Zurich, amesema: “Ningependa kuchukua nafasi hii kukupa pongezi zangu
dhati. Nakutakia kila la kheri katika majukumu yako.”
Rais wa FIFA amesema kwamba hana shaka na uwezo wa Karia hasa
ikizingatiwa kuwa alikuwa Makamu wa Rais wa kipindi kilichopita, hivyo atakuwa
fursa thabiti ya kuiletea nchi maendeleo ya mchezo soka.
“Kwa wakati wote, nakuhakikishia ushirikiano wa kutosha kutoka
FIFA katika malengo yako. Milango ya FIFA iko wazi wakati wowote wewe kuja
kujadili masuala ya mchezo wa mpira wa miguu hasa eneo la utawala.
“Ningependa kuchukua nafasi hii kukualika kuja hapa Zurich
wakati wowote kuanzia sasa ambako nitapata fursa ya kukutambulisha maeneo
mbalimbali ya FIFA. Nimeagiza upande wa utawala kuwasiliana nawe kuona na
kupanga tarehe rasmi ya safari,” amesema na kuongeza:
“Nikutakie tena kheri na fanaka, nguvu
na kila aina ya mafanikio katika majukumu yako mapya huku nikitarajia ujio wa
kuonana nawe haraka.”
Wakati huo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (FERWAFA)
nalo kwa upande wake wamempongeza Rais wa TFF, Wallace Karia kwa kuchaguliwa
kuwa kiongozi mpya wa shirikisho.
Katika barua ya FERWAFA iliyosainiwa na Rais wa shirikisho hilo,
Nzamwita Vincent imesema kwamba Rwanda itaendelea kuwa bega kwa bega na
Tanzania katika maendeleo ya mpira wa miguu kwa ushirikiano baina ya nchi mbili
kadhalika ukanda wa Afrika Mashariki unaounda Baraza la Sola la nchi za Afrika
Mashariki.
No comments: