Header Ads

Headline
recent

Masau Bwire aionya Simba





TIMU ya soka Ruvu Shooting yai Pwani imesema kuwa imetumia mchezo wa Ngao ya Jamii kuwasoma wapinzani wao Simba kwa ajili ya mchezo wao wa kesho Jumamosi wa ufunguzi wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema kocha mkuu wao Abdulhumud Haji ametumia mchezo huo kuwasoma Simba ipasavyo na atazifanyia kazi mbinu zao ili kushinda mchezo huo.

“Kocha wetu mkuu Abdulhumud Haji aliifuatilia Simba kwa ukaribu, tunahitaji watanzania waone jinsi tunavyofanya ili wawe na imani na timu yetu kutokana na kushinda mchezo huo kwani tutakuwa na heshima kutokana na timu tutakayokutana nayo ndiyo ipo juu kwa sasa.


“Timu yetu ipo vizuri, wachezaji wamecheza mechi nyingi za kirafiki na kila tuna imani ya kufanya vizuri dhidi ya simba hiyo kesho,” alisema Masau.

No comments:

Powered by Blogger.