Hawa Ndiyo Viongozi Wapya wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF)
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini, wakili Revocatus Kuuli ametangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa chama hicho uliofanyika leo katika Ukumbi wa Hosteli za Chuo cha Mtakatifu Gasper mjini Dodoma.
Revocatus
Kuuli wakati akitangaza matokeo ya nafasi ya urais wa TFF amesema
kwamba jumla ya kura zilizopigwa ni 128 ambapo kura halali ni 125 na
kura zilizoharibika ni 3.
Katika
kura hizo 125, Wakili kuuli alimtangaza Rais mpya wa Shirikisho hilo
kuwa ni Wallace Karia ambaye ameshinda nafasi hiyo kwa jumla ya kura
95 kati ya kura halali 125 zilizopigwa. Wagombea wengine wa Urais
pamoja na kura walizopata kwenye mabano ni Ally Mayay Tembele (9),
Shija Richard (9), Iman Madega (8), Frederick Mwakalebela (3) na
Emmanuel Kimbe (1). Ndugu Michael Wambura amechaguliwa kuwa Makamu wa
Rais wa Shirikisho hilo.
Wajumbe
wa Kamati ya Utendaji walioshinda kwenye uchaguzi wa leo pamoja na
Kanda wanazoziwakilisha kwenye mabano ni kama ifuatavyo:
Mohamed
Abeid (Dodoma na Singida), Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Sarah
Chao (Arusha na Manyara), Dustan Ditopile (Lindi na Mtwara), Elias
Mwanjala (Mbeya na Iringa), Francis (Pwani na Morogoro), Vedastus
Lufano (Mara na Mwanza), Lameck Nyangaya (Dar es salaam), Kenneth
Pesambili (Rukwa na Katavi), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga),
Issa Mrisho (Kigoma na Tabora) na James Patrick (Njombe
Rais
wa Shirikisho hilo, Wallace Karia, Makamu wa Rais, Michael Richard
Wambura pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa
wameapishwa leo mjini Dodoma muda mfupi baada ya matokeo ya ushindi
wao katika uchaguzi huo kutangazwa.
Akitoa
hotuba yake muda mfupi baada ya kuapishwa kwake, Rais wa Shirikisho
hilo (Wallace Karia) amesema kuwa amepigiwa simu na Rais wa
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino pamoja na Rais wa
Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad na wote wamelipongeza
Shirikisho hilo kwa uamuzi ulioufanya na kuutakia uongozi mpya
mafanikio mema.
No comments: