Hizi Ndizo Sababu za Chelsea Kupokea Kipigo cha 2-3 Kutoka kwa Burney
Mbio za kutetea taji zimeanza vibaya kwa Chelsea baada ya Gary Cahill na Cesc Fabregas kuoneshwa kadi nyekundu Sam Voakes akiwaadhibu mabingwa
Chelsea imeanza vibaya utetezi wao wa taji Ligi Kuu Uingereza kufuatia kichapo cha kufedhehesha kutoka kwa Burnley katika mechi ya ufunguzi wa ligi Jumamosi.
Gary Cahill akirithi kitambaa cha unahodha kutoka kwa John Terry, alitolewa mapema kwa kadi nyekundu katika uwanja wa Stamford Bridge baada ya kumchezea faulo mbaya Steven Defour na mambo yakaanza kuharibika kutokea hapo.
Blues walionekana kukosa furaha na kupoteza umoja, vijana wa Sean Dyche wakiwasambaratisha bila huruma.
Burnley walipata goli lao la kwanza, shukrani kwa Sam Voakes, mchezaji huyo aliifungia timu yake goli la pili kabla ya kwenda mapumziko.
Hata hivyo Alvaro Morata aliingia kwenye ubao wa magoli baada ya kuipatia Chelsea goli la kwanza dakika ya 69 hivyo kuwapa ari ya kupambana zaidi.
Conte ana kazi ya ziada sasa dhidi ya Tottenham Hotspur kwani wachezaji wake muhimu kama Cahill, Fabregas na Pedro hawatakuwepo.
Hizi ndizo Sababu zilizowaua Chelsea
1 Chelsea Walionekana bado hawajaimarisha
Chelsea wametumia fedha nyingi msimu huu kumsajili Alvaro Morata, Tiemoue Bakayoko na Antonio Rudiger, lakini wamepoteza wachezaji wengine.
Wakiwa na kibarua cha Ligi ya Mabingwa msimu huu, kukosekana kwa mcheka na nyavu Diego Costa na majeruhi Eden Hazard, kikosi chao kinaonekana kuwa dhaifu kiasi cha kutisha.
Meneja Antonio Conte alikuwa na hamasa ndogo kuligeukia benchi kuona ni nani ataokoa jahazi baada ya kunyukwa 3-0. Anahitaji msaada kutoka kwa mmiliki, vinginevyo Chelsea itakumbwa na zahma la msimu mbovu kama ule wa Mourinho.
2 Conte Alionekana kama anahitaji Kujaribu Kikosi chake
Kama inavyoonekana wazi kwamba Muitaliano huyo hana furaha kwa kushindwa kuwasajili wachezaji anaowataka, kilichoikumba Chelsea bila shaka kilikuwa kikitarajiwa.Kikosi cha kwanza hakijabadilika sana kutoka kile kilichotwaa ubingwa msimu uliopita na Burnley walicheza vizuri, wakati Chelsea ilitarajiwa kuifunga timu ndogo ya aina hii.
Conte anahitaji kuhamasisha wachezaji wake kufanya kazi licha ya uzito wa uongozi wa klabu kusajli wachezaji wapya.
3 Cahill na Fabregas Hawakuwa Makini Kwenye Mchezo Huo
Cahill alitwaa majukumu ya unahodha baada ya kurithi kitambaa kutoka kwa John Terry, na kwa ghafla amewaangusha wachezaji wenzake na meneja pia. Kukimbia hadi eneo la timu pinzani kujaribu kupokonya mpira kuisaidia timu yake kuutawala mchezo lilikuwa jambo jema, lakini faulo mbaya aliyocheza dhidi ya Defour ilikuwa hatari na refa hakuwa na uamuzi mwingine zaidi ya kumtunuku kadi nyekundu.Cesc Fabregas, ambaye alishaoneshwa kadi ya njano, alipewa haki yake ya kadi nyekundu kwa kucheza rafu mbaya isiyo ya msingi dhidi ya Jack Cork.
Chelsea sasa watawakosa wachezaji muhimu kuelekea mechi yao dhidi ya Tottenham, Leicester na Everton.
4 Chelsea Waliizarau Burnley Kwenye Mchezo Huo
Burnley maarufu kama Clarets walishinda mechi moja tu ugenini msimu uliopita, wakitegemea kuvuna pointi katika uwanja wao wa nyumbani zaidi, lakini wameonkana kuwa timu mpya katika uwanja wa Stamford Bridge.
Kufuatia kuondoka kwa Michael Keane na Andre Grey, wengi waliibeza Burnley na kuiweka kwenye kundi la timu za kushuka daraja.
Lakini Sean Dyche amethibitisha kuwa anaweza kuwa kocha mahiri zaidi katika Ligi Kuu Uingereza.
#Angalia Magoli Yote Hapa
No comments: