Header Ads

Headline
recent

Wachezaji Simba wamvuruga Omog



KOCHA Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog  amedai kuwa mpaka sasa bado hajui ni wachezaji gani watakao kuwa wakiunda kikosi chake cha kwanza kutokana na hali ya ushindani ilivyo ndani ya timu hiyo.

Omog amesema hayo wakati alipokuwa akizungumzia kuhusiana na uwezo wa wachezaji wake waliounyesha Jumanne iliyopita walipocheza na Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa kirafiki uliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Amelisema wachezaji wote katika kikosi chake wapo vizuri na kila mmoja amekuwa akionyesha kiwango cha juu kila anapopewa nafasi ya kucheza kwa hiyo jambo hilo limekuwa likimpatia wakati mgumu kupata kikosi cha kwanza.

“Kutokana na hali hiyo ninaweza kusema kuwa nina kazi kubwa ya kufanya ili kuweka mambo sawa na ni matumaini yangu kuwa hakuna kitakachoharibika.

 “Niwaombe tu Wanasimba wote kuendelea kutuunga mkono na kuwa bega kwa bega na sisi katika kutimiza mipango yetu yote tuliyojiwekea msimu huu,” alisema Omog.

No comments:

Powered by Blogger.