KOCHA KOEMAN ATIMULIWA EVERTON
KLABU ya Everton imetangaza kumfuta kazi kocha wa timu hiyo, Ronald
Koeman.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni saa chache baada ya timu hiyo
kukubali kichapo cha mabao 5-2 kutoka kwa Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu
England ‘Premier’ uliopigwa jana Jumapili katika Uwanja wa Goodison Park.
Makocha wanaotajwa kwenda kuchukua nafasi yake ni Kocha wa Burnley,
Sean Dyche, Eddie Howe (Bournemouth) na Marco Silva (Watford).
Leo asubuhi, kocha huyo kama kawaida alifika katika uwanja wa
mazoezi wa timu hiyo kwa ajili ya mazoezi ambapo alikutana na mwenyekiti wa
klabu hiyo, Bill Kenwright na Mtendaji Mkuu, Robert Elstone, wakafanya kikao.
Baada ya kikao hicho, mchana klabu hiyo ikatoa taarifa ya
kufukuzwa kwa kocha huyo ambayo ilisema: “Klabu ya Everton imethibitisha kwamba
Ronald Koeman ameondoka klabuni.
“Mwenyekiti, Bill Kenwright, bodi ya wakurugenzi na mwekezaji
mkuu, Farhad Moshiri, kwa pamoja wameridhika na huduma ya Koeman kwa kipindi
cha miezi 16 aliyokaa klabuni na kuisaidia timu kumaliza msimu uliopita nafasi
ya saba katika Premier.”
No comments: