Omog amchoka Mavugo, kuwekwa kiti moto
BENCHI
la ufundi la Simba limedai kuwa linahitaji kukaa na Laudit Mavugo raia ili
kumpa somo baada ya kuvurunda katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Hard Rock ya
Zanzibar Jumapili iliyopita.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Mavugo alivurunda vibaya jambo lilosababisha mashabiki wa Simba waanze kumzomea huku wakimshikiza kocha wao mkuu, Mcameroon, Joseph Omog amwondoe uwanjani.

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema kuwa, Mavugo ni mmoja wa wachezaji wazuri wanaowategemea ndani ya kikosi hicho na kudai kuwa kinachotokea ni mambo ya mpira hivyo wanahitaji kukaa naye kwa ajili ya kumjenga ikiwa ni pamoja a kumuandaa kisaikolijia ili aweze kuwa fiti zaidi.
“Tumefurahi kuona tumefanikiwa kushinda huu mchezo ambao tumeutumia kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Azam FC tutakaocheza nao Jumamosi, tunahitaji ushindi katika mchezo huo.
“Kuhusu mchezaji wetu Mavugo tunahitaji kukaa naye ili tuweze kumuelekeza nini cha kufanya na kumuweka sawa kisaikolojia kwani ni mchezazji mzuri na ana uwezo wa kufunga ambapo anahitaji kupewa maelekezo machache tu kwa ajili ya kumuweka sawa, hivyo tukikaa naye atakuwa vizuri,” alisema Mayanja.
No comments: