Kakolanya naye yupo fiti, sasa Yanga kicheko tu
BAADA
ya Obrey Chirwa na Amissi Tambwe kupona majeraha yao na kurejea kikosini Yanga,
kipa wa timu hiyo, Beno Kakolanya naye amepona na muda wowote anatarajiwa
kuanza mazoezi na wenzake.
Kakolanya
aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la goti la mguu wa kulia, alikaa nje ya uwanja
kwa zaidi ya miezi miwili tangu alipoumia akiwa na kikosi cha Taifa Stars
kilichoshiriki michuano ya Cosafa, Juni, mwaka huu nchini Afrika Kusini na
kushika nafasi ya tatu.
Kwa
takribani wiki mbili zilizopita, Kakolanya alikuwa akifanya mazoezi ya gym
baada ya kupewa programu maalum, ambapo programu hiyo aliimaliza jana Jumatatu
na leo Jumanne kwa mara ya kwanza alionekana katika Uwanja wa Uhuru, wakati
wenzake wakifanya mazoezi, lakini yeye akikaa nje.
No comments: