Header Ads

Headline
recent

Duu Huu Wimbo Mpya wa Roma Mkatoriki si Mchezo Aise!




Katika ngoma hiyo Roma ameongelea zaidi kuhusu tukio la kutekwa kwake, jinsi familia yake ilivyoteseka kumtafuta, pamoja na kuwashukuru wote waliopaza sauti zao katika jitihada za kumtafuta.

“Wengi mlijiuliza walioniteka ni maaskari mkanitafuta vituo vyote Central hadi Staki Shari, wakasema hawajui nilipo mama alienda hadi mochwari dah!

“Mwanangu alimuuliza mama baba lini atarudi? Na mke wangu aliwaliza kuwashukuru sina budi, kipi bora nife mseme nimekufa kiharakati, siogopi kufa ila nawaachaje wanaobaki?

“Kutekana tekana ni uhuni wa kishamba na waliosadiki Roma ataonekana kabla ya Jumapili, God bless imetimia injili niliyoitabiri”
Hiyo ni baadhi ya mistari inayopatikana kwenye wimbo huo wa Zimbabwe.

Tukio la Roma, msanii mwenzake Moni, na prodyuza wake Bin Laden kutekwa na watu wasiojulikana lilitokea miezi minne nyuma, ambapo tarehe 8 Aprili mwaka huu walirejea wakiwa na majeraha mwilini, na mpaka sasa kesi yao bado ipo katika vyombo vya sheria.

Download Hapa

No comments:

Powered by Blogger.