Haruna Niyonzima ndani ya nyumba Simba
Niyonzima (kushoto) akifanya mazoezi kwa kufuata maelekezo ya kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja. |
Mayanja akimnyoosha viungo, Niyonzima. |
Niyonzima akipiga 'kontroo'. |
Nduda akiwa amechumpa hewani kufuata moja ya mashuti aliyopigiwa. |
Niyonzima akimsalimia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe. |
KIKOSI cha Simba leo kimefanya mazoezi kwenye uwanja wa Boko Veterani uliopo Ununio jijini Dar ikiwa ni maandalizi ya bonanza lake la Simba Day linalotarajiwa kufanyika kesho Uwanja wa Taifa.
Katika mazoezi hayo kikosi hicho kiliwajumuisha wachezaji wake wapya akiwemo Haruna Niyonzima, John Boko, Emmanuel Okwi, Aishi Manula, Said Mohammed, Erasto Nyoni na wengineo.
Baada ya mazoezi hayo mashabiki waliofika kuangalia mazoezi hayo walishindwa kuzuia hisia zao na kuamua kulisukuma gari la Niyonzima huku wakimshangilia na kumkaribisha.
No comments: