Header Ads

Headline
recent

Campbell Awafariji Walemavu Nchini

Sol Campbell Akiwa kwenye picha ya pamoja na walemavu kwenye uwanja wa Karume, Dar es Salaam

Sol Campbell akiwa na walemavu


Sol Campbell akiwa na baadhi ya Walemavu



Sol Campbell akiwasili bongo
JUZI Jumamosi nyota wa zamani wa timu ya taifa ya England na klabu ya Arsenal, Sol Campbell alitua nchini kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ya mchezo wa soka baada kualikwa na Kampuni ya Mchezo wa Kubahatisha ya SportPesa.

Hata hivyo, mara tu baada ya kutua nchini, beki huyo alienda moja kwa moja kutembelea timu ya walemavu ya Muungano.

Akizungumza na wachezaji wa timu hiyo, Campbell baada ya viongozi wao kumwambia changamoto mbalimbali zinazowakabili aliwaambia kuwa wasikate tamaa na yupo pamoja nao ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao ikiwa ni pamoja na kuzishinda changamoto zinazowakabili katika maisha yao.

“Nashukuru sana kwa kukutana na nyinyi na ninawataka tu msikate tamaa kwa sababu ya ulemavu mlionao katika kupambana na maisha.

“Mnapaswa kujua kua maisha yenu ya baadaye yapo mikononi mwenu kwa hiyo hakuna haja ya kukata tamaa, mnatakiwa kupambana licha ya ulemavu mlionao, ni matumaini yangu kuwa tukishirikiana kwa pamoja tutashinda,” alisema Campbell kisha akawakabidhi vifaa wachezaji hao vifaa mbalimbali vya michezo vikiwemo, jezi pamoja na mipira.

No comments:

Powered by Blogger.